Uongozi wa klabu ya Yanga inayoshiriki ligi kuu soka Tanzania bara umetangaza orodha ya majina ya wajumbe wapya wa kamati ya ujenzi na miundo mbinu, sambamba na viongozi wawili wa kamati hiyo ya ujenzi kutoka Kamati ya Utendaji.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka klabuni humo inasema kamati ya utendaji ikiongozwa na mwenyekiti wake Dr. Mshindo Msolla imeteua wajumbe 18 ambao wameunda kamati hiyo ya miundombinu ambapo mwenyekiti wa kamati hiyo ni Mhandisi Bahati Mwaseba na makamu ni Dr Athumani Kihamia.

Pia taarifa hiyo imeainisha kuwa wajumbe ni Said Mrisho, Helieli Muhulo, Isaac Usaka, Jumanne Werema Abdallah Mrindoko, Buluba Mabelele, Gervas Kondombole, Hamad Islam, Ashura M. Ande, James Lobikoki, Peter Simon, Isaac Chanji, Said Hers, Fundi Sayore, Josephat Peter, Baraka Igangula, Suma Mwaitenda, Madaraka Marumbo.

Safari ya Yanga ya kutinga hatua ya makundi kwenye Ligi ya mabingwa Afrika ilikatishwa na Zesco siku ya jumamosi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kuwafanya kusonga mbele kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza uliochezwa hapa nchini.

Yanga baada ya kupoteza mchezo huo, sasa wameangukia kwenye kombe la shirikisho Afrika kucheza mechi za mtoano kusaka nafasi ya kutinga hatua ya  makundi.

TAKUKURU yataja ofisi za Serikali zenye kashfa ya Rushwa
Wawekezaji wapanga mikakati kupandisha thamani na soko la Maziwa nchini