Beki kisiki wa Young Africans Yao Kouassi pamoja na Mshambuliaji Kennedy Musonda huenda wakawa sehemu ya kikosi cha klabu hiyo kitakachoikabili SIngida Big Stars, baadae leo Ijumaa (Oktoba 27).

Miamba hiyo ya Ligi Kuu Tanzana Bara itakutana Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, huku kila upande ukiwa na lengo la kuzimiliki alama tatu za mchezo huo, unaotarajiwa kuwa na upinzani mkubwa.

Mshambuliaji Musonda alikosekana kwenye mechi tatu mfululizo dhidi ya Ihefu FC, Geita Gold na Azam FC, baada ya kusumbuliwa jeraha ya kifundo cha mguu ‘Enka’, huku Yao akiukosa mchezo dhidi ya Azam FC, kufuatia jeraha jeraha dogo lililokuwa likimsumbua.

Kocha Mkuu wa Young Africans Miguel Gamondi amethibitisha ufiti wa wachezaji hao kuelekea mchezo wa leo Ijumaa dhidi ya Singida Big Stars, hivyo atakuwa na wigo mpana wa kupangilia kikosi chake.

“Musonda kutokutumika kwenye mechi tatu mfululizo kunatokana na kusumbuliwa na jeraha la enka amepona, suala la kumtumika litategemea na namna atakavyokuwa kabla ya mchezo;

“Alikuwa sehemu ya mazoezi timu tangu Jumapili iliyopita lakini sikuona sababu za kumtumia dhidi ya Azam FC kutokana na kuhofia kumpa presha na akapata shida nyingine nikampa mapumziko.” amesema.

Akimzungumzia Yao, Kocha huyo kutoka nchini Argentina amesema pia alikuwa na shida ya enka aliumia kwenye mazoezini amerejea kikosini na anaendelea vizuri .

“Kila mchezaji ndani ya Young Africans ana umuhimu wake hivyo kurudi kwa wachezaji hao ambao wana mchango mkubwa ndani ya timu katika mechi sita tulizocheza naamini wataongeza nguvu na kasi ya kufikia malengo;

“Yao amehusika kwenye mabao mengi ya timu pia Musonda amefunga hivyo kurudi kwao wataongeza nguvu na kasi kutokana na kuwa na nguvu walizozitunza baada ya kukosekana kwenye michezo kadhaa.” amesema Gamondi

Musonda kwenye mechi sita walizocheza Young Africans yeye amecheza tatu, amefunga bao moja huku Yao akifunga bao moja na ametoa pasi tatu.

Mayele afunguka kuikataa Al Ahly, Mamelodi
Duke Abuya aichimba mkwara Young Africans