Madaktari katika mji mkuu wa Yemen Sanaa, wametoa ombi la dharura la kuokoa maisha ya mapacha wawili waliozaliwa Desemba 16, 2020 wakiwa wameungana.

Mkuu wa hospitali ya Al-Sabeen ambako watoto hao wa kiume walizaliwa amesema wako katika ‘hali hatari’ na wanahitaji upasuaji wa dharura ambao unaweza tu kufanyika nje ya nchi.

Mkuu huyo aliliambia Shirika la habari la AFP kuwa uchunguzi wa kimatibabu umeonesha kuwa mapacha hao wameunganika lakini kila mmoja ana moyo wake ingawa moyo wa mmoja wao uko katika hali ambayo si ya kawaida.

Aidha. ameeleza kuwa hospitali hiyo haina vifaa muhimu vinavyohitajika kutoa taswira kamili ya hali yao kuwa ni viungo gani vilivyounganika.

Uwanja wa ndege wa Sanaa ulifungwa kutokana na vita vya muda mrefu nchini Yemen, ambayo imeharibu kabisa miundombinu katika mfumo wa afya.

Shirika la misaada la mfalme Salman limeandika katika ukarasa wake wa Twitter uwezekano wa kujitolea kwake kusaidia hali ya watoto hao kuchunguzwa na wataalamu wa afya wa Saudi Arabia na kutathmini uwezekano wa kuwatenganisha mapacha hao.

Mhagama: Mameneja msiwasumbue wastaafu
Serikali yataifisha Almasi