Mwanaharakati Yericko Nyerere amethibitisha kusitisha mpango wa kuishtaki Young Africans mahakamani, kufuatia kukiuka kanuni za Ligi Kuu kwa kukataa kuvaa nembo halisi ya Rangi Nyekundu ya Mdhamini Bank ya NBC, ambaye ndiye Mdhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara ‘NBC PREMIER LEAGUE’
Yericko Nyerere ambaye aliwahi kuthibitisha kuwa yeye ni Shabiki na Mwanachama wa Simba SC, ameweka maelezo ya kusitisha mpango huo, kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Yericko ameandika: “Nimeliondoa kusudio la kuwafikisha Mahakamani @tanfootball, @nbc_tanzania na @yangasc aka Mazuzu ama Utopolo kwa kuvunja kanuni ya ligi kuu 16 kifungu cha 1:1.
Hii ni Baada ya Klabu ya @simbasctanzania kulete kocha mwenye sifa ya dunia Mr @pablofrancomartin, Kwa uungwana wa kibinadamu tu hasa kwa mtu mwenye kulitazama taifa kwa ajili ya kesho,
Nimeona kwa hekima na busara kwa kuwa klabu kubwa Afrika ya Simba imeingia gharama ya kuleta kocha ambae amewahi kufundisha @realmadrid ile Madrid ya @cristiano @sergioramos @marcelotwelve na magwiji wengine wa dunia, hakuna sababu ya kusimamisha ligi ili kumpiga ngumi za pua mjinga mmoja tu aitwaye Utopolo.
Naamini huko tuendako kwa kuwa Yanga bado wako gizani kwenye zama za mawe za kati, basi wataendelea kujifunza kwa Simba kila miaka inapokwenda. Simba iko mbele ya Yanga, TFF na wengine wote kwa miaka 40 mbele.
Hivyo nitaendelea kuwashauri Simba waendelee kutoa elimu ya bure kwa Yanga ili watoke kwenye lindi la ujinga huu ambao hautawafikisha kokote duniani.”