Mdau wa Michezo nchini Tanzania Yericko Nyerere amewasilisha ombi lake kwa Mwekezaji na Rais wa Heshima wa Simba SC Mohamed Dewji ‘Mo’, baada ya kukerwa na matokeo ya klabu hiyo msimu huu 2022/23.

Simba SC jana Jumapili (Mei 07) ilitolewa Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ kwa kufungwa na Azam FC katika mchezo wa Nusu Fainali uliopigwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Matokeo hayo yamehitimisha safari ya Simba SC msimu huu katika kusaka mafanikio ya kutwaa mataji, ambapo hadi sasa imefuta uhakika wa kutwaa taji lolote ambalo walilidhamiria msimu huu 2022/23.

Yericko amewasilisha ombi hilo, baada ya kumtakia kheri ya Siku ya Kuzaliwa Mohamed Dewji ambaye leo Mei 08 ametimiza umri wa miaka 48.

Yericko amemuomba Mo Dewji kuhakikisha anasafisha baadhi ya watu katika Uongozi wa Simba SC, ambao anaamini wanakwamisha mafanikio ya ndani ya Uwanja kwa kufanya usajili wa wachezaji kwa njia ya ubabaishaji.

Yericko ameandika: Heri ya kumbukizi ya kuzaliwa Tajiri @moodewji uishi miaka mingi sana bro! Nikuombe jambo moja kubwa sana tajiri, wewe ndio mwenye majority shares kisheria na ndie Mwenye timu na ndie mwenye maamuzi ya MWISHO, Safisha genge la wapigaji pale Simba linaloishi kwakutegemea utapeli wakati wa usajiri. Ubabaishaji pale Simba ni mkubwa na unaihujumu timu yetu.

Umefanikiwa kutuletea kocha mzuri sana mwenye ujuzi wa hali ya juu @robertinho7.coach , Sasa mpe nguvu ya kusajili timu, Ajili mtaalamu wa usajili wa wachezaji ili kuepuka madalali waliojazana pale klabuni. Mtaalamu huyu ashirikiane na kocha moja kwa moja katika kusajili wachezaji.

Viongozi/menejimenti imwache kocha afanye kazi yake, waache kumpangia kikosi, tumeshatoka zama hizo za kupangiwa timu. Wachezaji watimiziwe ahadi wanazoahidiwa katika mechi. Thamani ya wachezaji wa ndani ibadilike, walipwe maslahi mazuri yenye hadhi ya klabu ya Simba.

Happy birthday Boss na tajiri pekee wa mpira Tanzania uliyeleta mafanikio makubwa kuliko tajiri yoyote Tanzania na kusini mwa Jangwa la Sahara. Mafanikio ya mpira wa Tanzania kuanzia timu ya taifa na Vilabu, yako chini ya Account ya pesa ya tajiri Mohamed Dewji na sio vinginevyo.

Na Yericko Nyerere

Lehlogonolo Nonyane aitolea shombo Young Africans
Mashabiki Liverpool wazomea wimbo wa taifa