Beki Mkongwe nchini Tanzania Kelvin Yondani amesema kila zama kwenye soka zina wachezaji wake, hivyo ni jukumu la mchezaji kuhakikisha anafanya kitu cha kuacha rekodi za kusimuliwa na chipukizi wanaokuja nyuma yake.

Yondani ambaye kwa sasa anaitumikia Klabu ya Geita Gold FC amesema kitu kikubwa anachokiamini katika kazi hiyo ni nidhamu kuwa ndio msingi wa mafanikio kwa mchezaji anayejielewa.

“Kwanza mchezaji lazima ajue kwamba soka linaongoza kwa hisia kali za furaha na huzuni ndio maana wapo wanaofikia hatua ya kuzimia na wengine kupoteza maisha na mashabiki wanakuwa na imani kubwa na wachezaji wanaowawakilisha uwanjani”

“Hilo ni somo kubwa kwa mchezaji kufanya kazi kwa nidhamu itakayomfanya acheze kwa muendelezo wa kiwango kitakachoisaidia timu yake na mashabiki kupata burudani ya ujuzi wake wa kazi.”

“Jambo kubwa aliwashauri chipukizi wanaopata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao kuhakikisha wanavilinda ili visipotezwe na ustaa wanaoupata, wakiwa na mwanzo mzuri, huku wakitambua wazi kwamba mashabiki wanawajua kupitia kiwango na si vinginevyo.”

“Ndiyo maana kuna wachezaji wa zamani ambao walifanya makubwa wanasimuliwa hadi leo, hilo ni funzo kujua kwamba kazi ndizo ziliwapa heshima hadi leo, soka ni kazi ya thamani kwa wachezaji ambao wanajua thamani zao,” amesema Beki huyo ambaye aliwahi kutamba akiwa na Simba SC, Young Africans na Taifa Stars.

Baada ya kuachana na Young Africans misimu miwili iliyopita Kelvin Yondan Alitimkia Polisi Tanzania FC ambako alicheza kwa msimu mmoja.

Ismail Rage aingilia kati sakata la Fei Toto
Domayo atua rasmi Namungo FC