Beki wa Klabu ya Young Africans, Kelvin Yondani ameugomea Uongozi wa Klabu hiyo kuandika Barua ya kujieleza kwa nini asichukuliwe hatua za kinadhamu kutokana na kushindwa kwenda Ruangwa Lindi kucheza mchezo dhidi ya Namungo FC.
Yondani amesema hawezi kuandika Barua kwa sababu yeye aliomba ruhusa kutokana na matatizo ya kifamilia.
Wachezaji 6 wa Klabu ya Young Africans wametakiwa kuandika Barua za kujieleza kwa nini wasichukuliwe hatua za kidhamu kutokana na kushindwa kwenda kucheza mchezo dhidi ya Namungo kwa sababu mbalimbali.
Wachezaji hao ni Lamine Moro, Eric Kabamba, Mohamed Issa Banka, David Molinga Falcao, Kelvin Yondani na Haruna Niyonzima.
Inadaiwa kuwa Lamine Moro, Eric Kabamba na Mohamed Issa Banka waligoma kwenda kwa madai ya kuumwa Ila kocha alisema walikuwa wanachagua mechi huku David Molinga alikataa kwenda kwa sababu ya mke wake kujifungua wakati Haruna Niyonzima alikuwa na kadi Tatu Ila alihoji kuhusu Milioni 200 akasimamishwa na Uongozi wakati Yondani alisema ana matatizo ya kifamilia Ila Baada ya siku mbili akajiunga na Timu ya Taifa.
Katika mchezo wa Namungo FC, Young Africans walilazimishwa sare ya bao moja kwa moja, huku wakitangulia kupata bao dakika sita kupitia kwa Tariq Seif Kialala na bao la kusawazisha kwa wenyeji lilikwamishwa wavuni na Bigirimana Blaise kipindi cha pili.