Klabu ya Newcastle United imefanikiwa kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Japan, Yoshinori Muto baada ya kukamilisha mpango wa kupata kibali cha kazi cha mchezaji huyo wakati wote atakapokua England.
Klabu hiyo ya St. James’ Park imefanikisha na kumtangaza mshambuliaji huyo ambaye alikua akiitumikia klabu ya Mainz 05 ya Ujerumani kuanzia mwaka 2015.
Taarifa ya Newcastle Utd imeeleza kuwa, Muto amesaini mkataba wa miaka mitano ambao utamuweka klabuni hapo hadi mwaka 2023.
Muto anakua mchezaji watano kusajiliwa na meneja wa Rafael Benitez katika kipindi hiki cha dirisha la usajili wa majira ya kiangazi.
Wachezaji waliosajiliwa klabuni hapo kabal ya Muto ni Mikel Merino, Martin Dubravka, Fabian Schär and Sung-yong Ki.
Usajili wa wachezaji hao, una lengo la kuivusha Newcastle Utd katika malengo la kumaliza zaidi ya nafasi ya kumi walioishika kwenye msimamo wa ligi msimu uliopita, baada ya kurejea ligi kuu, wakitokea ligi daraja la kwanza.
Msimu huu klabu hiyo imepania kufanya makubwa zaidi ili kumaliza katika nafasi za juu ambazo zitawawezesha kushiriki michuano ya kimataifa barani Ulaya.
“Tuna matumaini makubwa, ujio wa mshambuliaji huyo utawezesha jambo kubwa katika kikosi chetu kuanzia msimu ujao wa ligi ya England.” Alisema Benitez
Muto anaweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kutoka nchini Japan kusajiliwa na The Magpies.
Newcastle United wataanza kampeni ya kusaka ubingwa wa Englamd msimu wa 2018/19 kwa kupambana na Tottenham Agosti 11.