Hatma ya kocha wa Young Africans, Hans Van Der Pluijm kuendelea na kibarua chake msimu ujao haijulikani kufuatia ukimya kutawala zoezi la kumpa mkataba mpya.

Hans amebakiza mwezi mmoja na Wanajangwani hao aliojiunga nao kwa mara ya pili mwishoni mwa mwaka juzi huku mazingira ya uondokaji wake mara ya kwanza na kutimkia Saudi Arabia yakifanana na haya ya sasa.

Taarifa kutoka ndani ya Young Africans zinaeleza ukimya uliopo juu ya kuanza majadiliano ya kumuongezea mkataba kocha Hans unatokana na kitendawili cha uchaguzi mkuu wa klabu.

Baada ya kuingoza Young Africans kubeba  taji la Ligi Kuu msimu uliopita pamoja na kuelekea kutetea taji msimu huu wengi wanaamini kuwa Hans anastahili mkataba mpya lakini kinachosumbua kichwa ni sintofahamu ya kama mwenyekiti, Yusuph ataendelea kuiongooza klabu baada ya uchaguzi kufanyika.

Hans yupo tayari kuendelea kuifundisha Young Africans lakini viongozi wa klabu wamekuwa wakimpiga danadana kuhusiana na kumpa mkataba mpya.

Tayari klabu kadhaa barani Afrika ikiwemo klabu moja kubwa nchini Tanzania inanyemelea huduma za kocha huyo raia Uholanzi mwenye uzoefu mkubwa wa soka la barani Afrika.

Nani Kutangulia Fainali Ya Ligi Ya Mabingwa Barani Ulaya Leo?
Kanisa Katoliki lachomwa moto