Uongozi wa wa Young Africans umeweka wazi kuwa kila mchezo kwao ni muhimu kupata ushindi bila kujali ni aina gani ya mashindano, hivyo watapambana kushinda kwenye mchezo wao ujao dhidi ya Mtibwa Sugar.

Young Africans chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi inakibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar, unaotarajiwa kuchezwa wikiendi hii ukiwa ni mchezo wa kwanza ndani ya ligi kwa Young Africans ndani ya Desemba.

Ni keshokutwa Jumamosi (Desemba 16), mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex, ambapo Mtibwa Sugar hawajawa kwenye mwendo mzuri baada ya kukusanya pointi tano kwenye ligi baada ya kucheza mechi 12.

Ofisa Habari wa Young Africans, Ally Kamwe amesema kuwa kila mchezo ni muhimu kupata matokeo kutokana na umuhimu wake.

“Tupo wenye ligi ya mabingwa Afrika na ligi ya ndani michezo yote ina umuhimu wake na tunaipa kipaumbele kikubwa, bila kujali tunacheza na mshindani wa aina gani kikubwa ni nidhamu na wachezaji kupambana kupata matokeo.

“Wachezaji wanatambua kile ambacho kinahitajika hivyo mashabiki mwendelezo wao wa kujitokeza kwenye mechi zote za Young Africans uendelee kwa kuwa wanakuja kushuhudia burudani,” amesema Kamwe.

Mfumo NeST kuwazibia wapigaji
MAKALA: Vidole visitumike kumkatili mama mtandaoni