Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Obrey Chirwa anatarajiwa kuwasili leo Dar es Salaam kukamilisha usajili wake kujiunga na Young Africans.

Chirwa alikuwa mshambuliaji pacha wa Donald Ngoma katika klabu ya FC Platinums ya Zimbabwe.

Na baada ya Ngoma kuhamia Young Africans, akawashauri viongozi wa timu hiyo wamchukue winga huyo wa kulia wa timu ya vijana ya Zambia chini ya umri wa miaka 23.

Na inaaminika Young Africans imekubali kutoa zaidi ya dola za Kimarekani 100 000 kuipata saini ya Chirwa ambaye anatokea FC Platinum ya Zimbabwe, klabu waliyotokea wachezaji wake wengine, Wazimbabwe Thabani Kamsuoko na Ngoma.

Mwaka jana, Chirwa alikataa kujiunga na Hobro IK ya Denmark kwa kutoridhishwa na malipo – na maana yake Young Africans itakuwa imempa mshahara mzuri.

Young Africans inataraka kutuma jina la mchezaji huyo Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ili awahi kucheza mechi za Kundi A Kombe la Shirikisho.

Na mpango huo utafanywa mapema tu atakapokamilisha usajili wake leo akiwasili.

Yalivyoripoti Magazeti Ya Ulaya Kuhusu Usajili
Kozi Ya Ukocha Yasogezwa Mbele Kupisha Mwezi Mtukufu