Kikosi cha Young Africans na benchi la ufundi linaloongozwa na kocha Zlatko Krmpotic, kinatarajia kuondoka Dar es salaam kesho Al-Khamis kuelekea mjini Bukoba, tayari kwa mchezo wa mzunguuko watatu wa Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar.

Mchezo huo utaunguruma Jumamosi Septamba 19 majira ya saa kumi jioni, kwenye Uwanja wa Kaitaba ulioko Bukoba, mkoani Kagera.

Meneja wa Young Africans, Hafidh Saleh, amesema katika kukijenga vema kikosi chao kuelekea mchezo huo wa kwanza wa ugenini, leo usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini, Dar es Salaam, walitarajia kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mlandege kutoka Zanzibar.

“Tutacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mlandege, hii itampa kocha Zlatko mwanga wa kuona maelekezo yake aliyowapa wachezaji mazoezini walivyoyafanyia kazi, itamsaidia kiufundi kubaini mahali walipoimarika na idara inayohitaji kuboreshwa,”

“Tunatarajia kuondoka jijini kesho na kuelekea Bukoba huku wachezaji watu wote wakiwa ‘fiti’ kwenda kupambana kusaka ushindi dhidi ya Kagera Sugar ambayo pia imekuwa ikitusumbua kila tunapokutana.” Amesema meneja huyo.

Young Africans itakutana na Kagera Sugar ambayo imetoka kulazimisha sare ya bila kufungana dhidi ya Gwambina FC kwenye Uwanja wa Gwambina Complex, wakati wao wanakumbukumbu ya ushindi wa bao moja kwa sifuri dhidi ya Mbeya City.

Michezo mingine ya mzunguuko watatu ya VPL itakayochezwa mwishoni mwa juma hili.

Chanzo ajali iliyoua watano Mtwara
Kenya yasalimu amri watanzania kukaa karantini