Uongozi wa Young Africans, umeweka wazi kuwa, wapo mbioni kutoa jezi mpya kwa ajili ya michuano ya kimataifa baada ya timu hiyo kufanikiwa kutinga katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.
Afisa Habari wa Young Africans, Ally Kamwe, amesema: “Baada ya kufanikiwa kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, sasa tunatarajia kuzindua jezi zetu za maana ambazo ni maalumu kwa ajili ya michuano ya kimataifa.
“Jezi hizo zitakuwa jezi kali kuliko hata jezi za msimu huu ambazo tayari zimeshatoka, kwa mfano jezi ya kijani mpya kwa ajili ya mashindano ya kimataifa ni jezi kali ambayo haijawahi kutokea kutokana na kuwa na ubora mkubwa.”
Young Africans imefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka 25.