Mkurugenzi wa Sheria wa Klabu ya Young Africans Wakili Patrick Simon amethibitisha taarifa za Klabu hiyo kupokea ofa kadhaa zinazomlenga Kiungo kutoka visiwani Zanzibar Feisal Salum ‘Fei Toto’.

Kiungo huyo amekuwa na matatizo na Uongozi wa Young Africans tangu mwishoni mwa mwaka 2022, akishinikiza kuvunja mkataba wake, lakini Maamuzi ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ yamemtaka Feisal kurejea klabuni hapo kwani bado ana mkataba halali.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Yanga TV Wakili Patrick Simon amesema: “Klabu mpaka sasa imepokea ofa kadhaa kuhusu kumtaka Feisal, lakini huwezi kuja moja kwa moja kwa klabu wakati hujui mchezaji yuko wapi.

“Kwa hiyo ofa ni kweli zipo na sisi tumewashauri walioleta ofa kuwa mchezaji hayuko na sisi na hajawa na sisi muda mrefu.”

“Kwa hiyo wamfuate mchezaji, wakubaliane naye makubaliano binafsi, kisha watakuja kwetu nasi tutawapa ofa yetu, tukikubaliana tutakuwa tayari kumwachia.”

Mkwasa aichambua Simba SC Vs Young Africans
Jasmin Razack: Feisal ana haki ya kuvunja mkataba