Ratiba hiyo ineonyesha watani wa jadi katika soka la Bongo Simba SC na Young Africans watakutana uso kwa macho Oktoba 18 kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo wa mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo, Young Africans ndiyo watakuwa wenyeji huku kila timu ikiwa imesajili wachezaji wapya wa ndani na nje.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB), Almas Kasongo amesema mchezo huo utachezwa huku timu zote zikiwa na uwiano sawa wa michezo.

“Kwa maana ya ‘big match’ (mechi kubwa) baina ya Yanga na Simba itachezwa Tarehe 18, Oktoba. Huu utakuwa ni mchezo wa raundi ya saba ya ligi na utachezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 11.00 jioni.

Msimu uliopita, timu hizo zilipokutana mzunguko wa kwanza zilitoka sare ya bao mawili kw amawili  wakati mzunguko wa pili Young Africans walishinda bao moja kwa sifuri, wakati mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), Simba walishinda bao manne kwa moja.

Kwa mwaka huu, timu hizo itakuwa ni mara ya nne kukutana ambapo mchezo wa mzunguko wa kwanza msimu uliopita ilichezwa Januari 4, mchezo wa mzuunguko ulichezwa Machi 8 wakati ASFC ilikuwa Julai 12 na hii ya msimu mpya itakuwa Oktoba 18.

Kichapo chamchefua Harry Maguire
Mganda kusajiliwa Simba Queens