Wakati ligi kuu ya soka Tanzania bara ikisimama kupisha michuano ya Kombe la Challenge itakayoanza kutimua vumbi lake mwishoni mwa juma hili, mabingwa wa soka nchini Young Africans wameanza kujiandaa kisaiolojia, pindi ligi hiyo itakaporejea tena baadae mwezi Desemba.

Young Africans watacheza dhidi ya Mbao FC katika mchezo wa mzunguuko wa 12 wa ligi kuu ya soka Tanzania bara, na tayari imefahamika watamkosa kiungo mshambuliaji Ibrahim Ajib ambaye tangu alipojiunga na wakali hao ameonyesha uwezo wa hali ya juu.

Ajib ambaye ni sehemu ya wachezaji wanaounda kikosi cha Tanzania bara (Kilimanjaro Stars) kitakachoshiriki michuano ya Kombe la Challenge mwaka huu, atakosa mchezo dhidi ya Mbao FC kutokana na adhabu ya kadi tatu za njano alizozipata kwenye michezo ya ligi iliyopita.

Viongozi wa benchi la ufundi la timu hiyo chini ya kocha wake mkuu, Mzambia George Lwandamina, wanaumiza vichwa jinsi gani watakavyo kabiliana na hali hiyo, kutokana na umhimu wa Ajibu kikosini kwa sasa.

 Ajibu alipata kadi ya tatu ya njano katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons siku ya jumamosi, uliochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.

Tayari, Meneja wa Young Africans Hafidh Saleh, amethibitisha juu ya suala hilo.

Manara autamani Urais
Azam FC wafunga milango ya usajili