Mzunguuko wa 19 wa ligi kuu ya soka Tanznaia bara umekamilishwa rasmi hii leo kwa mchezo mmoja kuchezwa katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara kati ya Ndanda FC waliokua wenyeji wa mabingwa watetezi Young Africans kutoka Dar es salaam.
Dakika 90 za mchezo huo zimekamilika kwa Ndanda FC kukubali kufungwa nyumbani mabao mawili kwa moja yaliyopatikana katika dakika za 36, 40 na 46.
Young Africans ndio walikua wa kwanza kupata mbao la kuongoza kupitia kwa Hassan Kessy kabl ya kiungo kutoka Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo Papii Kabamba Tshishimbi hajaongeza bao la pili kwa njia ya Panati, huku Nassoro Kapama akiifungia Ndanda FC bao la kufutia machozi.
Kwa ushidni huo Young Africans wanafikisha poinr 41, nakuendelea kuwafukuza wapinzani wao katika soka la bongo Wekundu wa Msimbazi Simba walio kileleni kwa kumiliki point 45.
Mzunguuko wa 20 wa ligi kuu ya soka Tanzania bara utaanza rasmi siku ya ijumaa kwa mchezo kato ya Wekundu wa Msimbazi Simba ambao watakua nyumbani Dar es salaam dhidi ya Stand Utd kutoka mkoani Shinyanga.