Klabu ya Young Africans imekanusha taarifa zinazovumishwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kuachwa kwa baadhi ya wachezaji itakapofika mwishoni mwa msimu huu.

Taarifa iliyotolewa na Katibu mkuu Young Africans Charles Boniface Mkwasa imeeleza kuwa, hakuna ukweli wowote wa taarifa za kuachwa kwa wachezaji, na huenda zina malengo ya kuanza kuwavuruga katika kipindi hiki cha kuelekea mwishoni mwa msimu.

“Taarifa hizo ni za uongo na uzushi mkubwa . Uongozi upo bega kwa bega na wachezaji wote 27 na benchi lao la ufundi. Hatujakaa kulijadili hilo wala kulifikiria bali tupo makini kutetea ubingwa wetu wa ligi kuu.”

“Mwenye maamuzi ya mwisho juu ya huduma ya wachezaji klabuni kwetu ni kocha mkuu Mr George Lwandamina na timu yake sio kiongozi mwingine yoyote na kocha huyo hajatoa taarifa yoyote ya kumwacha mchezaji gani au yupi kumuongezea mkataba zaidi ya kila siku kuukazania uongozi kuboresha masilahi yao kwa sababu kama kocha mkuu anajivunia na kujali kazi ya vijana wake.” Imeeleza taarifa ya Katibu mkuu wa Young Africans.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, wachezaji wote ni muhimu na uongozi Young Africans unajivunia kwa moyo wao thabiti kuitumikia klabu. Hivyo wamewaomba wachezaji kuwapuuza watoa habari feki za klabu, na badala yake waendelee kucheza kwa bidii.

Young Africans Kujipima Geita
Liverpool Yajidhatiti Nafasi Ya Tatu