Mratibu wa klabu ya Union Maniema ya DR Congo Guy Kapya Kilongozi amesema klabu ya Young Africans imezidiwa dau na klabu ya TP Mazembe katika kumsajili kiungo mshambuliaji Mercey Vumbi Ngimbi.

Young Africans ilikua inatajwa kukaribia kumsajili kiungo huyo kutoka DR Congo, tangu juma lililopita.

Kilongozi amesema nyota huyo atajiunga na TP Mazembe badala ya Young Fricans, kufuatia klabu ya Union Maniema kupokea dau nono kutoka Lubumbashi.

Ngimbi mwenye umri wa miaka 24 alitaka kujiunga na Young na si TP Mazembe.

Young Africans walikuwa wamekubaliana kila kitu na walitakiwa kutoa dau la dola 40,000 (milioni 92.7 za Kitanzania) kwa Maniema na mshahara wa dola 2,600 kwa mwezi (milioni 6 za Kitanzania) kwa Ngimbi.

Baada ya Mouse Katumbi kusikia kuwa Ngimbi amekataa kujiunga na TP Mazembe kwa sababu ya Young Africans alikubali kulegeza masharti ya mkataba na kumpelekea mkataba wa miaka 3 wenye mshahara wa dola 4,000 kwa mwezi (milioni 9.2 za Kitanzania) na akatoa dau la dola 100,000 (milioni 231.9 za Kitanzania) kwa Maniema.

Waziri Ummy awataka Wakuu wa Mikoa kusimamia ukusanyaji mapato
Shabiki wa Simba SC awasili Dar es salaam