Klabu ya Young Africans imeanza vyema Msimu wa Ligi Kuu 2021/22 kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar, waliokua nyumbani Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.
Bao la Young Africans katika mchezo huo lilifungwa na kiungo kutoka visiwani Zanzibar Feisal Salum *Fei Toto* dakika ya 23 kipindi cha kwanza.
Kwa ushindi huo Young Africans inaungana na klabu za Mbeya Kwanza FC, Polisi Tanzania, Mbeya City FC, Namungo FC ambazo zimeshinda michezo ya mzunguuko wa kwanza wa Ligi hiyo ambao umefikia tamati baadaya mchezo wa Kaitaba.