Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Injinia Hersi Said ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindao Young Africans, amesema wanaendelea na mchakato wa kusaka kocha mpya atakayerithi mikoba iliyoachwa na Cedric Kaze

Kumekuwa na tetesi kumuhusu kocha wa zamani wa Harambee Stars na Guinea ya Ikweta Sebastian Migne anayetajwa kumalizana na mabingwa hao wa kihistoria katika soka la Bongo.

Hersi amesema Migne ni miongoni mwa makocha wanaofanya nao mazungumzo lakini bado hawajafikia muafaka wa kimaslahi.

“Ni kweli, Migne ni miongoni mwa makocha ambao tuko katika mazungumzo nao, lakini hayuko peke yake, wengine wapo pia. Bado mwafaka haujafikiwa kuamua yupi tumkabidhi timu, ” amesema Hersi

Awali Young Africans ilikuwa na mpango wa kumuachia timu kocha Juma Mwambusi mpaka mwishoni mwa msimu huu, huku kazi kubwa ikiwa ni kuhakkisha anaiwezesha klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitatu.

Hata hivyo wamebadili ‘gia angani’ wakiamua kumleta kocha mpya ambaye atafanya kazi na Mwambusi ili hata pale ligi itakapomalizika atakuwa amefahamu uimara na madhaifu ya timu yako wapi ili imsaidie katika kufanya maboresho.

Kocha Kaze alionyesha mlango wa kutokea baada ya kikosi cha Young Africans kulazinishwa sare ya 1-1 dhidi ya Polisi Tanzania mjini Arusha, mchezo ambao ulitanguliwa na kichapo cha 1-0 kutoka kwa Coastal Union ya jijini Tanga.

KMC FC waisukia mipango Young Africans
Rais Samia aagiza vyombo vya habari vilivyofungwa vifunguliwe