Wakati ukimya kikiendelea kutawala kuhusu usajili wa wachezaji watakaojiunga na klabu ya Young Africans kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, klabu hiyo kongwe katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati inaendelea kuhusishwa na mpango wa kuwawinda baadhi ya wachezaji wa ndani na nje ya nchi.

Young Africans ambayo kwa sasa imepoteza matumaini ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kutokana na upinzani mkali uliopo kati yake na Simba SC, inahusishwa kumsajili beki wa kushoto wa KMC FC, David Brayson.

Bryson amekuwa akiitwa katika kikosi cha Taifa Stars tangu akiwa kikosi cha Gwambina FC msimu uliopita aliposajiliwa na timu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja ambao mwisho wa msimu huu unamalizika.

Taarifa zinaeleza kuwa Young Africans wapo kwenye hatua za mwisho kumsaini Bryson, ili kuja kuwa chaguo la kwanza katika nafasi ya beki wa kushoto ambayo tangu ameondoka, Gadiel Michael hakuna aliyefiti kwa uhakika.

Young Africans kama watafanikiwa kumpata Bryson, maana yake kati ya Adeyun Saleh au Yassin Mustapha mmojawapo amaweza kuachwa.

Wakati huo huo klabu hiyo inatajwa kumuwinda kiungo mshambuliaji wa Simba SC Ibrahim Ajib, ambaye mkataba wake ndani ya Wekundu hao wa Msimbazi utafikia kikomo mwishoni mwa msimu huu.

Ajib anahusishwa kuondoka Simba SC, kufuatia kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza, huku iielezwa kuwa ameshindwa kabisa kumshawishi kocha Mkuu Didier Gomes kumpa nafasi ya kuanza mara kwa mara.

Rais Samia asisitiza watanzania kujikinga na corona
Waziri Mkuu aagiza matumizi ya nishati mbadala