Mabosi wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans wanadaiwa kuifanyia umafia Simba SC kwa kupanda dau kwenye kuipata saini ya beki wa Ihefu FC, Yahaya Mbegu, ambaye taarifa zinasema amemalizana na Singida Big Stars.

Sasa baada ya taarifa hizo kuwepo, Young Africans wenyewe wametua huko Singida kuhamisha usajili huo kabla ya jina lake kuingizwa kwenye mfumo wa usajili wa Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’.

Mbegu alijiunga na Ihefu FC msimu huu, na kujihakikishia namba katika kikosi cha kwanza, jambo ambalo timu nyingi zimeanza kumpigia hesabu.

Chanzo cha habari kutoka Dar es salaam kinaeleza kuwa, Young Africans ilikuwa ikimvizia Mbegu mapema tu, ila baadaye ikasikia Singida Big Stars pia wanamtaka kabla ya Simba SC nao kupeleka ofa yao, ambapo iliamua kuongeza nguvu kwa Singida ili baadae ikamsajili kutokea huko.

“Simba SC walikuwa wanamtaka sana Mbegu na walifanya kila aina ya mbinu ili kumsajili, lakini baada ya Young Africans kuingilia dili hilo iliamua kuwaongezea pesa Singida Big Stars wamalizane naye, kisha hapo baadae ikamsajili kutokea huko kabla ya jina lake kupelekwa TFF.

“Usajili wetu hautamaliza mambo ya kimafia hata siku moja, maana kila kukicha vimbwanga vya kunyang’anyana wachezaji kati ya Simba SC na Young Africans haviishi na hasa kwenye usajili wa dirisha hili lijalo tutaona mengi sana,” kimeeleza chanzo hicho

Dodoma Jiji yatamba kuivurugia Namungo FC
Kocha Namungo FC aitaka nafasi ya tano Ligi Kuu