Ligi kuu ya soka Tanzania bara imeendelea tena hii leo kwa mchezo mmoja wa mzunguuko wa 18 kati ya mabingwa watetezi Young Africans ambao walikua nyumbani uwnaja wa Uhuru jijini Dar es salaam kuwakabili Majimaji FC kutoka mkoani Ruvuma.
Dakika 90 za mchezo huo zimemalizika kwa Young Africans kuibuka na ushindi wa mabao manne kwa moja.
Young Africans walipata bao la kwanza kwa njia ya mkwaju wa penati iliyotokana na beki wa Majimaji Fc Mpoki Mwakinyuke kuunawa mpira katika eneo la hatari kwa makusudi, hali ambayo ilipelekea kuonyeshwa kadi nyekundu na mwamuzi wa mchezo huo.
Peneti hiyo ya Young Africans ilikwamishwa wavuni na kiungo kutoka Jamuhuri Ya Kidekrasia Ya Kongo Papii Kabamba Tshishimbi karika dakika ya 17.
Bao la pili la Young Africans lilipatikana katika dakika ya 29 kupitia kwa mshambuliaji kutoka nchini Zambia Obrey Chirwa baada ya kumalizia vizuri kwa kichwa mpira wa krosi ya uliopiugwa na beki wa pembeni Gadiel Michael huku mshambuliaji Emmanuel Martine aliongeza bao la tatu kwa kuachia mkwaju mkali katika lngo la Majiamaji FC katika dakika 43.
Majimaji walipata bao la kufutia machozi katika dakika ya 56 kwa njia ya mkwaju wa penati uliokwamishwa wavuni na Marcel Kaheza, baada ya Said Makapu kuunawa mpira katika eneo la hatari.
Dakika ya 85 Young Africans waliandika bao la ushindi kupitia kwa Tshishismbi aliyepiga shuti kali nje ya 18, na kuelekea moja kwa moja kwenye lango la Majimaji FC.
Kwa ushindi huo Young Africans wanafiisha Point 37 na kuendelea kushika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara, wakitanguliwa na Simba wenye point 41.
Kesho ligi hiyo itaendela kwa mchezo mwingine mmoja wa mzunguuko wa 18 kati Wekundu wa Msimbazi Simba ambao watakua wageni wa Mwadui FC, kwenye uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.