Kocha Mkuu wa Simba SC Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesema, atakaa chini na nyota wa timu hiyo akiwemo Clatous Chama na Jean Baleke ili kuzungumza nao waongeze hali ya utulivu wanapokuwa ndani ya 18 kwa kufikiria haraka zaidi.

Simba SC ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 63 baada ya kucheza michezo 26 tofauti ya alama tano dhidi ya Young Africans yenye alama 68 kileleni.

Robertinho amesema kwenye kila mechi ambazo wanacheza kumekuwa na makosa ambayo yanajitokeza mara kwa mara kutimia nafasi wanazopata.

“Clatous Chama, Baleke, Ntibazonkiza (Saido) ni wachezaji wazuri tutaongea nao kwenye uwanja wa mazoezi ili kuboresha makosa, na yale mazuri kuyaendeleza zaidi kwenye michezo yetu.”

“Unajua kwenye mpira kikubwa ni nafasi na namna ya kuwakabili wapinzani ikiwa una mpira ni lazima ufanye maamuzi ya haraka kwa kuamua kufunga ama kutoa pasi ya bao.”

“Hilo limekuwa kwa wachezaji wetu wanapokuwa uwanjani kama uliona mchezo wetu dhidi ya Young Africans kuna nafasi tulikosa za kufungwa kwa wachezaji wetu hilo tumeona na tutafanyia kazi,” alisema kocha huyo raia wa Brazil.”

Hofu yatanda Nigeria, VAR tishio Young Africans
ASA kuzalisha tani 4,000 za mbegu msimu wa Kilimo