Uongozi wa klabu ya Young Africana umetoa taarifa ya kushtushwa na chaguo la mwamuzi wa kati Ahmed Arajiga wa Manyara kuchezesha mchezo wa Fainali Kombe la Shirikisho (ASFC) dhidi ya Simba SC, mchezo ambao utachezwa Jumapili July 25 mjini Kigoma.
Young Africans imeliomba Shirikisho la Soka nchini “TFF” na menejimeti ya mashindano kutafakari juu ya uamuzi wa kumtumia mwamuzi huyo kwenye mchezo wa Fainali kwani mashaka na hofu yao kwa mwamuzi huyo ni kuchezesha michezo ya Simba SC hatua ya Robo, Nusu na sasa amepangwa kwenye Fainali.
Ahmed Ragija alitangazwa jana Jumatano (Julai 22), kuwa Mwamuzi wa mchezo wa Fainali Kombe la Shirikisho.