Kiungo mshambuliaji Jimmy Ukonde Julio aliyekuwa akiichezea UD Songo ya Msumbiji amewasili Dar es salaam kimya kimya, huku akihusishwa na mpango wa kuwa mbioni kusajiliwa Young Africans.
Kiungo huyo ambaye alicheza sanjari la Luis Miquissone alipokua UD Songo ya Msumbiji, ambayo iliitoa Simba SC hatua ya awali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu wa 2019/20.
Jimmy anakua mchezaji wapili kutoka nje ya Tanzania kuwasili Dar es salaam akitanguliwa na Mshambuliaji kutoka DR Congo Fisyon Mayele ambaye aliwasili jana Jumamosi mchana.
Jimmy atakua na mazungumzo na viongozi wa Young Africans baadae leo Jumapili (Agosti Mosi) jijini Dar es salaam, na kama mambo yatakwenda sawa atasaini mkataba wa miaka miwili.
Young Africans imejizatiti kufanya usajili wa kiwango utakaoboresha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu na Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.