Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Bodi ya Ligi ‘TPLB’ Karim Boimanda amekiri kupokelewa kwa malalamiko kutoka kwa Wadau wakiilalamikia klabu ya Young Africans kuvunja kanuni kwa kuvaa Jezi nyeusi mfululizo.
Young Africans imefululizo kuvaa Jezi za rangi nyeusi kwa Michezo ya nyumbani na ugenini ya Ligi Kuu, halia mbayo imeleta tahariki hadi malalaiko hayo kufikishwa Bodi ya Ligi ‘TPLB’.
Boimanda amesema jambo hilo litafanyiwa kazi na kama Young Africans watakuwa wamevunja kanuni, na adhabu yake ni faini Shilingi milioni moja.
Ameongeza klabu zinatakiwa zivae Jezi kulingana na jinsi walivyozitambulisha, Nyumbani, Ugenini na Jezi ya Tatu ambayo unaruhusiwa kuvaliwa sehemu yoyote ikiwa imetokea mgongano wa rangi za Jezi na pinzani.