Uongozi wa Klabu ya Young Africans, umetangaza kuwa makini katika michezo ya Ligi Kuu (NBCPL) na Kombe la Shirikisho (ASFC) msimu huu 2021/22, ili kufikia malengo waliojiwekea.

Uongozi wa klabu hiyo kongwe katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati umetangaza kuchukua tahadhari ya kuwa makini wakati wote, kufuatia michezo michafu inayodaiwa kufanya katika mapambano ya kusaka ubingwa wa Tanzania Bara kila msimu.

Mmoja wa Viongozi wa ndani wa klabu hiyo ambaye hakutaka jina lake lianikwe hadharani amesema, wameshtukia mbinu chafu zinazopangwa na wapinzani wao kwa sasa, hasa katika kipindi hiki ambacho wanajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Azam FC ambao utachezwa Jumamosi (Oktoba 30).

Mchezo huo utachezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, huku Young Africans ambao hawajapoteza mchezo wowote mpaka sasa wakitarajiwa kuwa wenyeji.

Kiongozi huyo amesema: “Kuna watu wanafanya hujuma ili Yanga waweze kufeli kwenye mzunguko wa kwanza na kutoka kwenye malengo ya ubingwa kama ilivyokuwa msimu uliopita.”

“Viongozi hivi karibuni walikaa na wachezaji ambao hawapati namba kwenye kikosi kwa ajili ya kushirikiana kuhakikisha ubingwa unarejea nyumbani msimu huu.”

“Wanaotuhujumu tumeshagundua na kwa sasa wanataka kuanza kwenye mechi inayofuata dhidi ya Azam FC.”

Young Africans inashika nafasio ya pili katika msimamo wa Ligi kuu Tanzania Bara kwa kufikisha alama 9 baada ya kucshinda michezo mitatu, sawa na Polisi Tanzania iliyo kileleni.

Simba SC kumfahamu mpinzani wake leo
Mambo manne kumng'oa Gomes Simba SC