Uongozi wa Young Africans umetamba kuwa na kikosi imara kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ na Michuano ya Kimataifa inayoratibiwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’.

Afisa Habari wa Klabu hiyo Kongwe katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati Hassan Bumbuli amesema, kuelekea msimu ujao hawana wasiwasi wowote kuhusu kikosi chao, kwani usajili uliofanywa umeongeza makali zaidi.

Bumbuli amesema kwa uhalisia Young Africans itaendelea kutamba katika Soka la Tanzania na imedhamiria kushangaza kwenye Michuano ya Afrika, ambapo watashiriki Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Amesema wanaamini hata sasa kikosi chao kinaweza kucheza mchezo wowote wa ndani ama nje ya nchi na kikafanya vizuri, licha ya kutoanza kambi ya Maandalizi ya msimu ujao.

“Timu yetu iko vizuri, Tumesajili vizuri, sisi Wachezaji wetu wanaweza wakaja siku yoyote, wakakusanyika alafu tukaenda uwanjani na kikapigwa na mtu akaumia vilevile,” amesema Bumbuli Kikosi cha Young Africans kinatarajiwa kuanza Kambi ya Maandalizi ya msimu mpya leo Jumatano (Julai 20), Avic Town Kigamboni jijini Dar es salaam.

Zakazakazi amkataa Bernard Morrisons
Aishi Manula mitatu tena Simba SC