Mabingwa wa soka Tanzania bara Young Africans, wapo tayari kwa mshike mshike wa michuano ya kombe la shirikisho la soka barani Afrika CAF, kufuatia kutuma majina na wachezaji wanne waliowaongeza kwa ajili ya michuano hiyo.

Hassan Kessy na Juma Mahadhi ni kati ya majina yaliyotumwa kwenye ofisi za shirikisho la soka barani Afrika CAF zilizopo mjini Cairo nchini Misri.

Kessy alijiunga na klabu hiyo kongwe hapa nchini akitokea kwa Wekundu wa Msimbazi Simba, baada ya mkataba wake kufikia kikomo na Mahadhi ametokea kwa Wagosi Wa Kaya, Coastal Union ya jijini Tanga.

Young Africans pia imeongeza majina mengine mawili ya kiungo Andrew Vicent ‘Dante’ aliyetokea Mtibwa Sugar pamoja na Beno Kakolanya ambaye amejiunga nao akitokea kwa maafande wa jeshi la Magereza Tanzania Prisons ya jijini Mbeya.

Awali, Young Africans walipeleka majina 24 CAF, hivyo kuongezeka kwa majina hayo manne, maana yake ni majina 28 na inaendelea kubaki na nafasi mbili.

Michael Carrick Kuutumikia Utawala Wa Jose Mourinho
Ukawa wamjibu Naibu Spika, ‘Posho akawatishie watoto’