Baada ya kuitoa Club Africain ya Tunisia na kutinga Hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Afrika, Shirikisho la Soka Barani humo ‘CAF’ limeirudisha tena Klabu ya Young Africans katika nchi hiyo ya Afrika kaskazini.
Young Africans ambayo itashiriki hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho baada ya miaka kadhaa kupita, imepangwa Kundi D na klabu ya US Monastirienne ya nchini Tunisia.
Klabu nyingine zilizopangwa na Young Africans kwenye Kundi hilo ni TP Mazembe (DR Congo) na AS Real de Bamako (Mali).
Makundi mengine ya Michuano hiyo yaliyopangwa leo Jumatatu (Desemba 12), Kundi A lina timu za USM Alger (Algeria), Marumo Gallants FC (Afrika Kusini), Al Akhdar SC (Libya) na FC Saint Eloi Lupopo (DR Congo).
Kundi B: ASEC Mimosas (Ivory Coast) Diables Noir (Congo Brazzaville), Rivers United FC (Nigeria) na DC Motema Pembe (DR Congo).
Kundi C: Pyramids (Misri), ASKO Kara (Togo), Future (Misri) na ASFA Rabat (Morocco).