Uongozi wa klabu ya Young Afrucans, umethibitisha kuzungumza na Shirikiaho la Soka nchini (TFF) ili kuwapata wachezaji wao walioitwa kwenye timu ya taifa Taifa Stars.

Kwa sasa Taufa Stars ipo kambini ikijiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia, dhidi ya DR Congo.

Uongozi wa Young Africans umelazimika kuzungumza na TFF ili kuwapata kwa muda mchache wachezaji wao kwa ajili ya kutambulishwa na kushiriki katika tamasha la siku ya Mwananchi, litakalofanyika kesho Jumapili (Agosti 29), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi wa Mashindano wa Young Africans, Thabit Kandoro amesema TFF imeafiki kuwaachia kwa muda wachezaji wao, hivyo hawana budi kurudisha shukurani kwa kuwatimizia hilo.

“Tayari tumeshaongea na uongozi wa timu ya taifa ya Tanzania juu ya kuwaomba wachezaji wetu wote katika mchezo wa kilele cha siku ya Mwananchi dhidi ya Zanaco FC na tayari ombi letu limekubaliwa.” amesema Kandoro.

Mbali na mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki, Tamasha la siku ya Mwananchi litapambwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wakiongozwa na Koffii Olomide.

Watekelezaji mfumo wa ukaguzi wa mifugo waonywae
Kompany, Silva wajengewa sanamu jijini Manchester