Klabu ya Young Africans, wana Jangwani wamewaomba radhi wadhamini wao wakuu, SportPesa kwa kutovaa jezi yenye logo yake, jana.
Kupitia taarifa yao kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Klabu hiyo, Charles Mkwasa, Klabu hiyo imeeleza kuwa ilifanya kosa hilo kwenye mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya USM Alger nchini Algeria.
Imeeleza kuwa kosa hilo lilifanyika kutokana na kukosekana kwa maelekezo ya matumizi ya jezi ya wadhamini, hali iliyosababisha kuziba sehemu yenye wadhamini hao.
Wana Jangwani wamesema kuwa ili kuondokana na kosa hilo katika mechi zijazo, wanafanya utaratibu kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili waweze kutumia nembo hiyo ya SportPesa.
Soma taarifa kamili: