Klabu ya Young Africans imeweka rekodi ya kuingiza Mashabiki wengi zaidi kwa msimu wa 2020/21, ambao ulifikia tamati mwezi Julai 2021.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mapema hii leo na Bodi ya Ligi Tanzania Bara (TPLB), imeeleza kuwa Young Africans iliingiza Mashabiki wengi zaidi, kwenye michezo yake ya nyumbani iliyochezwa jijini Dar es salaam.
Taarifa hiyo imeonesha Young Africans kwa msimu mzima iliingiza mashabiki 141,681, ikifuatiwa na Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC iliyoingiza mashabiki 138,518 na Dodoma Jiji FC inashika nafasi ya tatu kwa kuingiza mashabiki 27, 455.
Wakati huo huo Bodi ya Ligi Tanzania Bara (TPLB imetoa orodha ya klabu ziliyoingiza mapato mengi ya mlango kwenye uwanja wa nyumbani msimu wa 2020/2021.
Katika Orodha hiyo bado Young Africans inaongoza kwa kujizolewa Shilingi 986,826,000, ikifuatiwa na Simba SC iliyoingiza Shilingi 929,705,000 huku JKT Tanznaia inayoshika nafasi ya tatu ikipata Shilingi 148,145,000.