Rapa Young Killer Msodoki, ameamua kufuata nyayo za aliyekuwa Rais wa Libya, Muammar Gaddafi kwa kuamini katika uwezo na uimara wa wanawake katika kutoa ulinzi thabiti.

Rapa huyo amempa ajira mwanamke mmoja kuwa mlinzi wake binafsi, baada ya kuridhishwa na uwezo wake wa kushiriki mapambano makali.

Akizungumza kupitia XXL ya Clouds FM, rapa huyo kutoka Mwanza ameeleza kuwa uamuzi wake haukuwa ‘kiki’ na kwamba lilianza kama wazo kuwa angependa awe na mlinzi binafsi wa kike, na wazo lake likakamilika baada ya rafiki yake mmoja kumpendekezea mwanamke ambaye alikubaliana na uwezo wake. Hivi sasa, Killer anatembea na mwanamke huyo ambaye pamoja ni kwamba ni ‘kifaa haswa’, tabasamu lake ni adimu.

“[Kilichofanya nikubali uwezo wake] mapambano ambayo ameshawahi kuyafanya kwenye ulingo na kuwakalisha watu, kwenye kickboxing,” Young Killer aliiambia XXL.

Msodoki amekuwa mtu wa kwanza mwanaume maarufu Tanzania kuwa na mlinzi binafsi mwanamke anayezunguka naye sehemu mbalimbali.

Hatua hii ni sawa na alivyokuwa marehemu Gaddafi ambaye alikuwa Rais pekee duniani wakati huo aliyekuwa analindwa na jeshi la wanawake mahiri kwenye mapambano ya aina zote.

Gaddafi alikuwa akiamini katika uwezo wa wanawake na aliwapa nafasi kubwa jeshini. Wasichana walikuwa wakipatiwa mafunzo ya kijeshi tangu wakiwa shuleni.

Aliamini kuwa wanawake wanapoamua kuwa watiifu wanakuwa watiifu kweli na hujitoa maisha yao kwa ajili ya kiongozi wao. Wanawake waliofanikiwa kufuzu vizuri mafunzo walikuwa sehemu ya walinzi wake aliozunguka nao duniani kote, na unaambiwa ilikuwa ‘gusa unate’. Gaddafi alikuwa akitajwa kuwa mmoja wa viongozi wenye ulinzi mkali zaidi Afrika.

Hadi anauawa mwaka 2011, jeshi la wanawake waliokuwa wakimlinda lilipigana na maadui zake hadi tone la mwisho lakini wengine walikamatwa.

Muammar Gaddafi akipewa ulinzi mkali na kikosi cha wanawake akiwa na aliyekuwa Rais wa Ukraine, iktor Yushchenko alipoitembelea Kiev

Hata hivyo, wanawake hao hawakuwahi kupewa nafasi ya kujiunga na vikosi vya makomando kutokana na ukweli wa maumbile na mafunzo mazito ya kikomando. Lakini kupitia makala moja maalum, mmoja wa wakufunzi wa wanawake hao alieleza kuwa wanaamini ipo siku moja wao pia watakuwa sehemu ya kikosi maalum cha makomando.

Ni hatua nzuri kwa Young Killer kuamini kuwa wanawake na wanaume wote uwezo wetu uko sawa, inategemea mafunzo uliyochukua. Usichanganye kwa Young Killer kisa mlinzi wake ni mrembo, nikujuze tu ni bingwa wa mapambano ya ngumi na mateke (kickboxing) ‘UTAPIGWA UTACHAKAA!’

 

View this post on Instagram

 

AREA TODAY #MLINZ_AKIMUANGALIA_MLINZI_ ? ? by @venus__pictures ?

A post shared by ᎷᏚOᎠOKI (@youngkillermsodokii) on

Vuta pumzi, angalia ngoma yake mpya ‘Nahisi’.

Rais amkaanga mkandarasi aliyechelewesha ujenzi kituo cha mabasi Njombe
Rais Magufuli atoa siku 30 kituo cha mabasi Njombe kukamilika