Kama ukitaja habari ya michezo nchini ambayo inazungumzwa zaidi kwa sasa huwezi kuacha kuitaja habari ya Yusuph Manji kujiuzulu nafasi yake ya Uenyekiti wa klabu ya Yanga.

Maamuzi hayo yanatajwa yalichukuliwa na Manji baada ya kuona kuwa anashutumiwa vibaya na watu mbalimbali wakiwepo viongozi wa serikali na viongozi wengine wa Yanga hivyo kukaa pembeni ili kulinda heshima yake.

Jambo hilo lilionekana kupokelewa vibaya na mashabiki na wanachama wa Yanga kwani Jumanne ya Agosti, 17 walikutana katika makao makuu ya klabu yao na kukubaliana kumsimamisha uanachama Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali ambaye alidaiwa ndiyo aliyechochea Manji kuchukua uamuzi huo baada ya kuzungumza katika vyombo vya habari kuwa Manji amekurupuka.

Baada ya hayo yote, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Habari wa Yanga, Jerry Muro ametoa taarifa kutoka kwa Manji ambayo amemwagiza aifikishe kwa mashabiki wa klabu hiyo inayozungumzia hatma ya mahusiano yake na Yanga.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Muro aliandika “Jerry waambie wana yanga pamoja na vurugu zote hizi nitaendelea kuwa upande wao na kamwe sitawaacha nguvu yangu iko kwa wanachama,wapenzi na mashabiki”- Bw Yusuf Manji”

Paul Makonda Kuwapokea Hilal Hilal Na Magdalena Moshi
Simba SC Yavunja Mkataba Na Janvier Besala Bokungu