Winga wa klabu ya Crystal Palace, Wilfried Zaha amesema hajutii uamuzi wa kuchagua kuichezea timu ya taifa ya Ivory Coast na kuitosa Uingereza.

Zaha mwenye umri wa miaka 24 alikuwa katika kikosi cha kwanza cha Uingereza chini ya miaka 21 akicheza kama nahodha katika mchezo dhidi ya Sweden mwezi Novemba mwaka 2012 na katika mchezo dhidi ya Scotland mwezi Agosti mwakan 2013.

Hata hivyo baada ya kutoitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza ya wakubwa kwa miaka minne, mwaka 2016 Zaha ambaye alizaliwa mjini Abidjan alichagua kucheza timu ya taifa ya Ivory Coast.

”Ni kama nilikataliwa katika timu ya Uingereza, miaka minne katika mpira ni mingi sana sijutii kwani hakuna yeyote aliyenifikiria,” alisema Zaha.

Zaha aliiambia CNN Sport kuwa pamoja na kwamba Ivory Coast aitoshiriki katika michuano ya kombe la Dunia mwaka huu bado hajutii maamuzi yake kwani wanajipanga kufanya vizuri katika michuano ijayo.

 

Mwalimu amdhalilisha kingono mwanafunzi shule ya msingi
Urusi 2018: Nani atabeba Kombe? Tuimulike Ujerumani