Baada ya kushindwa kupata ushindi kwenye michezo mitano ya Ligi Kuu Bara, Kocha Mkuu wa Coastal Union, Mwinyi Zahera amesema kuwa amekerwa na matokeo hayo anarudi kwenye uwanja wa mazoezi kuangalia amejikwaa wapi kwa kuangalia madhaifu ya kikosi chake.

Coastal Union wanashika mkia kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi mbili baada ya michezo mitano wakitoka sare mara mbili na kufungwa michezo mitatu.

Wagosi wa Kaya wamepoteza dhidi ya Azam FC 1-0, Simba SC mabao 3-0 na kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Dodoma Jiji huku ikiambulia suluhu mbele ya Tabora United na sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar.

Kocha Zahera amesema kuwa kama mwalimu hafurahishwi kabisa na kipindi anachopitia hivi sasa baada ya kushindwa kupata ushindi kwenye michezo mitano iliyopita anarudi kujipanga kwa ajili ya michezo ijayo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Hakuna mwalimu anayependa kuona anashindwa kupata matokeo katika michezo mfululizo, hivyo nimeyaona mapungufu ya kikosi changu naenda kuyafanyia kazi makosa yote yaliyojitokeza katika michezo iliyopita ili tuweze kurudi kwenye ubora wetu,” amesema Zahera.

Mkutano FAO wamfikisha Waziri Mkuu Italy
Jack Wilshere aitwa Marekani