Nchini Bangladesh zaidi ya Watu 37 wamepoteza maisha na wengine wapatao 100 wamejeruhiwa baada ya kivuko kilichokuwa kimejaa watu kushika moto na kuteketea

Maafisa wa eneo hilo la kusini mwa Bangladesh wamesema moto huo ulianza katikati ya mto karibu na mji wa Jhalakathi ikiwa baadhi yao walifariki baada ya kuruka na kuzama katika maji.

Taarifa zinasema kuwa moto huo uianzia chumba cha injini na kusambaa maeneo mengine kwa haraka.

Idadi ya waliofariki katika maafa hayo huenda ikaongezeka kwa sababu abiria wengi walioungua wapo katika hali mbaya.

Taarifa za awali zinaripoti kuwa takribani watu 500 waliingia ndani ya kivuko hicho mwanzo wa safari ikiwa ni pamoja na maafisa 310.

Odinga asherehehekea Sikukuu na Watoto wahitaji
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Disemba 24, 2021