Zaidi ya watu Bilioni 3.9 kote Duniani wamekuwa wakifuatilia tukio la kuagwa mwili wa aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt John Pombe Magufuli.

Hayo yameelezwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa wakati akizungumza katika tukio la kuagwa mwili wa Hayati Dkt Magufuli katika Uwanja wa Amaan, Unguja Visiwani Zanzibar.

“Kwa taarifa tulizonazo mpaka jana jioni zaidi ya Watu Bilioni 3.9 karibu Watu Bilioni 4 Duniani walikuwa wanafuatilia tukio la kumuaga Hayati Magufuli Kitaifa jana Dodoma na naamini leo pia itakuwa hivyo, tunawashukuru Waandishi wa Habari kwa kazi nzuri” amesema Waziri Mkuu.

Mwili wa Hayati unaagwa Visiwani Zanzibar leo Machi 23, 2021 na kesho Machi 24 utaagwa Mkoani Mwanza na kisha baadaye kupelekwa Chato, mkoani Geita.

Mkwasa aahidi mazito Ligi Kuu
Garzitto: Soka la Afrika linanuka rushwa