Rapa mahiri kutoka kwenye kiwanda cha muziki nchini Zaiid, siku chache zilizopita ameiachia rasmi orodha ya nyimbo zake takriban 20 zitakazopatika kwenye album yake mpya inayotarajiwa kutoka siku za hivi karibuni.
Muda mfupi baada ya kuachia orodha hiyo, Jambo kubwa lililoibua mijadala kwa wadau wa muziki kote nchini, ni kitendo cha rapa huyo kutumia majina ya wasanii wakike kutoka katika tasnia ya muziki na filamu nchini kama majina rasmi ya nyimbo hizo.
Katika mahojiamo yake na XXL, Zaiid alifunguka dhamira ya yeye kufanya hivyo huku akiweka wazi kuwa moja ya sababu kubwa ni kudhihirisha kiwango cha heshima na thamani ya mwanamke.
“Kwanza kabisa mimi napenda wanawake, nimeona kuna haja ya kuwaheshimisha wanawake, ikiwa kama kijana, na nikiwa kama kioo. Kwa sababu mwisho wa siku, sisi wote tumetoka kwa wanawake.
Nikasema nahitaji kufanya kitu kwa wanawake, nikiamini kinaweza kuwapa hiyo heshima, nilivyokuwa nikiwaza hivyo nikasema ngoja nianze kwa kutumia majina yao ili kuakisi uhaliasia wa ninachotaka kukiongea.
Basi nikaanza kutengeneza wimbo mmoja baada ya mwingine, ilikuwa iwe EP, lakini kutokana na majina kuwa mengi na nina mawazo mengi ya kuwakilisha nikajikuta nimengeneza nyimbo zaidi ya 20 kiwangi cha Album.” Alisema Zaiid.
Kupitia kwenye ukurasa wake maalumu wa mtandao wa Instagram rapa Zaiid alichapisha orodha hiyo ambapo wimbo wa kwanza ameupa jina la ‘Shishi Food’ ambao tayari ameuachia.
Nyingine ni 2. ‘Kajala’ 3. Zuchu 4.Jojo 5.Hamisa 6.Wema 7.Lulu 8. Hadija Kopa 9. Grace matata 10. Ruby 11. Maua 12. Isha Mashauzi 13. Salama 14. Saraphina 15. Tunda 16. Chemical 17.Baby Madaha. 18.Lina 19.Stara 20. Witness.