Rais Samia Suluhu Hassan amesema uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam utaifanya iwe na uwezo mkubwa na ufanisi zaidi, wa kuwahudumia wateja wake kutoka popote Duniani.

Rais Samia ameyasema hayo kwenye hotuba yake kama mgeni rasmi wa maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Zambia, iliyofanyika Ikulu ya Lusaka.

Aidha, Rais Samia pia aliitumia nafasi hiyo kuishawishi Serikali na Wafanyabiashara wa Zambia, kuendelea kuitumia Bandari ya Dar es Salaam kama kituo chake Kikuu cha usafirishaji na upakuaji wa mizigo yake.

Awali, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliungana na Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema kuweka mashada ya maua kwenye Mnara wa uhuru wa Zambia ikiwa ni ishara ya kutoa heshima na kutambua walioongoza harakati za kuliletea uhuru Taifa hilo mwaka 1964.

TFF yamgusa Rais wa FIFA
Man City, Liverpool zagongana kwa Musiala