Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema amemshukuru Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipa nchi hiyo hekta 20 za ardhi kwa ajili ya kuhudumia mizigo ya nchi hiyo.

Rais Hichilema amesema hayo wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari alioufanya na Rais Dkt. Samia kwenye Ikulu ya Zambia, iliyopo jijini Lusaka.

Rais wa Zambia, Haikande hichilema.

Rais Hichilema alisema, Wazambia wamechukua hatua hiyo kama zawadi ya kuonyesha ushirikiano mwema baina ya nchi hizi mbili.

Katika hotuba yake akiwa ni mgeni rasmi wa maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Zambia yaliyofanyika jana Oktoba 24, 2023 jijini Lusaka, Rais Samia alisema eneo ambalo Zambia itapewa liko Kwala, Mkoani Pwani.

Gamondi ahisi harufu ya ubingwa Tanzania Bara
Usiku wa Madini: Miss Tanzania kivutio onesho bidhaa za Vito, Usonara