Mamlaka ya Maendelo ya Zambia (ZDA), imepiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki kwa wananchi yake na kutoa fursa mpya za biashara kwa kutengeneza mifuko inayoweza kutumiwa zaidi ya maramoja.
Kiongozi wa ZDA, Perry Mapani, ameeleza kuwa marufuku hiyo inatarajiwa kuchochea uvumbuzi katika sekta ndogo ya ufumaji wa vikapu ambavyo vanaenda na wakati na vinadumu kwa muda mrefu na kutoa nafasi zaidi ya ajira.
” Wakati umefika sasa wa kufufua ajira ya ufumaji wa vikapu katika Nchi yetu ambavyo tunategemea vitatengenezwa kwa ubunifu na kutumia vifaa asilia” amesema Mapani.
Aidha, amesema marufuku hiyo ianze kutekelezwa maramoja na pia itasaidia kampuni zinazotumia zaidi ya dola milioni 30 za kimarekeni kila mwaka katika kuagiza bidhaa za ufungishaji kupunguza gharama za uendeshaji.
Hata hivyo, Zambia ni ni miongoni mwa nchi zinazopakana na Tanzania zilizopiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki, ambapo nchi nyingine ni nchi ndogo ya Rwanda.