Chama tawala nchini Zimbabwe cha ZANU-PF kimewafukuza wabunge 11 waliokuwa wakimuunga mkono hadharani aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Robert Mugabe, huku rais Mnangagwa akiendelea kuchukua hatua dhidi ya maafisa waliowaunga mkono hadharani, Robert Mugabe na mkewe Grace,

Taarifa iliyotolewa na Naibu Spika wa bunge la nchi hiyo, Mabel Chinomona imesema kuwa ZANU-PF imeliarifu bunge kuwa wabunge hao 11 kwa sasa hawawakilishi maslahi ya chama hicho,

Aidha, mwezi Novemba mwaka jana, chama hicho cha ZANU-PF kilitangaza kufuta uwakilishi wa wabunge watano waliokuwa wafuasi wa karibu zaidi wa Mugabe, akiwemo Jonathan Moyo, ambaye alikuwa miongoni mwa wanasiasa waliokuwa kwenye kundi lililokuwa likimuunga mkono Grace Mugabe,

Hata hivyo, wafuasi wa Mnangagwa wamesema kuwa wana hofu na baadhi ya wafuasi wa Mugabe kama wataweza kuungana tena na kufanya kampeni dhidi ya rais huyo mpya katika uchaguzi ujao.

 

 

Majaliwa amsweka ndani Mkurugenzi
Mashabiki: Diamond katoa wimbo na Rick Ross kama hakijatokea kitu