Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Rais wa Jumuiya ya Waturuki waishio Ughaibuni, Abdullah Eren na ujumbe wake Ikulu Zanzibar tarehe 7 Desemba 2023.

Katika mazungumzo yao wawili hao wamegusia ushirikiano katika sekta elimu ikiwemo ufadhili wa masomo kwa wanafunzi 50 kila mwaka.

Masomo hayo ni kwa ngazi ya shahada, shahada ya uzamili na shahada ya uzamivu nchini Uturuki kuanzia mwakani 2024 pamoja na mafunzo kwa walimu wa vyuo vya amali na mengineyo.

Katika msafara huo, Rais huyo wa Jumuiya ya Waturuki waishio Ughaibuni aliambatana na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Dkt. Mehmet Gulluoglu.

Uongozi Mashujaa FC wakwepa shinikizo
Mwekezaji mpya Man Utd kuidhinishwa rasmi