Serikali ya Mapindizu ya zanzibar na Serikali ya Tanzania zimekutana kutia saini hati za makubaliano ya kuondoa changamoto Tano za Muungano ambazo zimeshapatiwa ufumbuzi.

Makamu wa Rais waTanzania, Samia Suluhu Hassan leo Oktoba 17,2020 ameongoza kikao cha kusainiwa kwa hati za makubaliano hayo.

Akizungumza baada ya kusainiwa kwa hati za kuondoa changamoto hizo, Makamu wa Rais amesema kwamba uwepo wa changamoto haumaanishi kuwa Muungano ni mbovu, kwani hata kwenye familia kuna migongano na njia ya kumaliza ni kupatiwa ufumbuzi.

Aidha, ameagiza changamoto nyingine sita ambazo bado hazijapatiwa ufumbuzi zijadiliwe na suluhisho lipatikane ili muungano huo uendelee kuimarika.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali hizo mbili wakiongozwa na makamu wa rais, Samia Suluhu Hassan na waziri mkuu, Kassim Majaliwa, waziri wa nchi, ofisi ya makamu wa rais (muungano na mazingira), Mussa Azzan Zungu ameyataja mambo hayo kuwa ni ushirikishwaji wa SMZ katika masuala ya kimataifa na kikanda, ushiriki wa Zanzibar katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mengine ni gharama ya kushusha mizigo katika bandari ya Dar es Salaam kwa mizigo inayotoka Zanzibar, utafutaji na uchimbaji wa mafuta ya gesi asilia na utaratibu wa vikao vya kamati ya pamoja ya kushughulikia masuala ya muungano.

Zungu amesema hatua hiyo inachangiwa na kikao cha kamati ya pamoja kwa ajili ya kushughulikia masuala ya muungano kuridhia hoja hizo tano za muungano zilizopatiwa ufumbuzi.

Ajinyonga baada kuzuiliwa kurudi usiku
Mbatia apinga kufungiwa kampeni