Timu ya taifa ya wanawake ya Zanzibar (Zanzibar Queens) hii leo imepoteza tena mchezo wa watatu kundi la kwanza katika michuano ya CEACAFA Challenge inayoendelea mjini Jinja nchini Uganda baada ya kukubali kufungwa mabao 11-0 dhidi ya Kenya.

Kipigo hicho kwa Zanzibar Queens kinakua cha tatu mfululizo ambapo kama itakumbukwa vyema katika mchezo wa mzunguuko wa kwanza hatua ya makundi walifungwa mabao 10 kwa 1 dhidi ya Burundi na kisha Uganda wakawabanjua mabao 9-0.

Kikosi cha Zanzibar Queens kinarejea nyumbani na huenda kikatumuia udhaifu wao kwa mwaka huu kwa ajili ya kujipanga na michuano ya CECAFA Challenge ya mwaka 2017.

UVCCM wavurugana Arusha
Video: Prof. Baregu apinga ripoti ya Twaweza, asema JPM anaminya demokrasia