Wizara ya afya Zanzibar leo Aprili 15, 2020 imetoa taarifa ya ongezeko la wagonjwa wapya wa virusi vya covid 19 ambao ni 6 na kufanya idadi ya wagonjwa kuwa 18 kutoka 12 ambao walitolewa taarifa Aprili 13.
Imeelezwa kuwa wagonjwa wote tayari wamelazwa katika vituo maalum kuendelea na matibabu.
Wagonjwa hao watanzania ni ; Mwanaume mwenye miaka 37 mkazi wa fuoni, mwanaume mwenye miaka 45 mkazi wa pangawe, mwanaume mwenye miaka 60 mkazi wa kwamchina, mwanamke mwenye miaka 48 mkazi wa migombani.
Mwanaume mwenye miaka 63 mkazi wa kijichi ambaye alifariki tarehe 11, nyumbani kwake na kuzikwa siku hiyo hiyo.
Huku mgonjwa mwingine aliyaathirika ni mwanaume raia wa Misri mwenye miaka 33 aliyeingia nchini Machi 15 akitokea kwao kwa kupitia Dubai.